Habari

IRINGA: Mgogoro wa ardhi wa mwaka 1992 watatuliwa 2019, “Tulipanga kwenda Dodoma kumuona Rais Magufuli”

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi saba dhidi ya chuo kikuu cha Iringa uliodumu toka mwaka 1992.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutatua mgogoro

Akizungumza kwenye ofisi za mkuu wa chuo hicho, DC Kasesela amesema kuwa amefanikiwa kuutatua mgogoro huo kutokana na kuzikutanisha pande mbili ambazo zilikuwa zinagombana kuhusu ardhi ya chuo hicho ilipochukuliwa mwaka 1992.

Huu mgogoro ni wa miaka mingi na mimi nimeukuta hivyo leo nimefanikiwa kuumaliza kwa njia ya busara kabisa kitu ambacho pale zilizokuwa zinalalamika zimefikia muafaka” alisema Kasesela.

Aidha, Kasesela amesema kuwa wamefanikiwa kumaliza mgogoro kwa kuwatafutia kila mmoja kiwanja kimoja ili kufidia maeneo ambayo serikali ilikipatia chuo kikuu cha Iringa.

Nimewaagiza uongozi wa chuo kuwa ikifika siku ya jumatatu waje ofisini kwangu ili wawalipe nauli zao hawa wananchi kwa kuwa wanawajibu kwa mujibu wa makubaliano yetu ambayo tulikuwa tumefikia kwenye kikao hiki, Kwa leo nimefalijika kuona familia hii imeamua kumaliza mgogoro huu ambao ulikuwa hauna afya katika harakati za kuleta maendeleo kwa wananchi hawa kwa kuwa walikuwa wanapoteza muda mwingi kupigania mgogoro huu,” Amesema Kasesela.

Kwa upande wa waliokuwa wanalalamika wakiwakilishwa na Mwaija Ngaga pamoja na Zuhura Balama walisema kuwa wameridhishwa na maamuzi yaliyofikiwa na kumpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa kwa kumaliza mgogoro huo.

Kwa kweli mkuu wa wilaya tunaomba ufikishe salamu zetu kwa Rais kwa kuchagua viongozi kama nyie wenye maono ya kushughulikia kero za wananchi maana la sivyo tulipanga kwenda Dodoma kumuona Rais Magufuli,” walisema wazee hao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents