Habari

Jaguar apandishwa kizimbani, kuendelea kusota mahabusu baada ya kukosa dhamana

Mbunge wa jimbo la Starehe, Kenya, Charles Njagua maarufu Jaguar Alhamisi hii amerudishwa rumande katika Kituo cha Polisi cha Kileleshwa baada ya kukosa dhamana huku Hakimu akisema atatoa hukumu Ijumaa

Wakati Hakimu Sinkiyan Tobiko akisema hayo, Mwendesha mashtaka wa Serikali ameiomba Mahakama kuwa Jaguar ashikiliwe kwa siki 14 katika Kituo cha Polisi cha Kamukunji ili kuwezesha kumalizika kwa uchunguzi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kituo cha habari cha Citizen Digital cha Kenya, makaratasi ya Mahamama yanasema hali ya kiintelijenisia inaonesha Jaguar alipanga kuunda kikundi cha Watu na kuvamia wageni waishio Kenya.

Mwendesha Mashtaka amesema kuwa Wapelelezi wamewaandikia Mamlaka ya Mawasiliano na wanafanya taratibu za kuviandikia vyombo vya habari ili kupata video inayomuonesha Jaguar na matamshi yake.

Aidha, Wapelelezi wameeleza zaidi kuwa wanashikilia simu ya mkononi ya Mbunge huyo ila bado haijafanyiwa uchunguzi wowote.

Source: Citizentv

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents