Burudani

Jay Moe awataja Diamond na Alikiba kama wasanii waliofanikiwa kimataifa

Msanii wa muziki wa Bongo, Jay Moe amewataja Diamond na Alikiba kama wasanii waliofanikiwa kimataifa kutoka Bongo.

Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Bata’ ameiambia XXL ya Clouds Fm ili msanii kutambulika amefanikiwa kimataifa ni lazima awe anafanya biashara ya muziki kwa upande huo pia.

“Msanii kwenda kimataifa ni kufanya biashara ya muziki ambayo itakuwa akiifanya kimataifa lakini mimi kufanya wimbo na msanii wa Marekani kwangu sioni kama nimeenda kimataifa labda hiyo project ikaleta matunda ya kimataifa,” amesema Jay Moe.

“Tumeona leo wasanii kama Diamond, Alikiba inasema yeah huu ni msanii ameenda kimataifa, why?, kwa sababu huu wimbo wa Aje na M.I umechukua tuzo mbili za kimataifa ambazo alishindana na wasanii wa mataifa mengine,” amesisitiza.

Jay Moe ameongeza kuwa msanii kufanya kolabo na msanii wa nje wakati msanii huyo hajivunii kazi hiyo bado si kwenda kimataifa vinginevyo hivyo kazi ilete matunda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents