Habari

Jeneza latelekezwa kwa imani za kishirikina

Waombolezaji katika Kijiji cha Katani wilayani Nkasi mkoani Rukwa wameitelekeza maiti kwenye jeneza na  kutimua mbio baada ya mvua kubwa iliyoambana na radi kuanza kunyesha ghafla.

Tokeo la picha la jeneza

Tukio hilo lilitokea jana saa 6 mchana wakati wanakijiji hao walipokuwa wanaenda kuzika na ndipo ghafla mvua kubwa iliyoambatana na radi na upepo mkali ilipoanza kunyesha kitu ambacho kiliwafanya waombolezaji kukimbia majumbani mwao kwa kuhofia kupigwa na radi.

Hata hivyo, Baadhi ya wananchi walivumilia nakurejea na jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu nyumbani na kuahilisha maziko kwa muda ili kupisha hali hiyo itulie na walikwenda kuzika baadaye katika makaburi yaliyopo kijijini hapo.

Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kaungo, Robert Kanoni, akizungumzia tukio hilo amesema wananchi wakiwa wanaelekea kufanya maziko ya marehemu aliyetambulika kwa jina la Dismas Kanoni, ghafla mvua kubwa  iliyoambatana na radi na upepo mkali ilianza hali iliyosababisha waombolezaji kuingiwa na hofu.

Bw. Kanoni amesema tukio hilo lilizua hisia za kishirikina kwa wananchi wa kijiji hicho kwani miezi miwili iliyopita baba yake na marehemu huyo alifariki baada ya kugongwa na gari la kampuni ya ujenzi wa barabara na walipofanya maziko siku iliyofuata walikuta ngozi ya kondoo juu ya kaburi la marehemu kitendo kilichowashangaza.

Akizungumzia hasara zilizotokana na mvua hiyo, Kanoni ameema kutokana na mvua hiyo, nyumba zipatazo 10 zimeezuliwa na nyingine kubomolewa kabisa na zinatakiwa kujengwa upya na wahanga waliopatwa na janga hilo tayari wamepatiwa hifadhi na misaada ya kibinadamu kwa wenzao.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya maafa ya wilaya ya Nkasi ambaye ni Mkuu wa wilaya, Ndg. Said Mtanda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kujenga makazi bora kwani miongoni mwa nyumba  hizo zipo ambazo zimeezekwa kwa nyasi.

Chanzo:Nipashe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents