Habari

Jeshi la polisi laingiza bilioni moja ndani ya wiki mbili kwa makosa ya barabarani

Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limekusanya Tsh bilioni 1.1 kuanzia Novemba 10 hadi Novemba 23 kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani.

Kamanda Mambosasa

Kiasi hicho cha fedha kimepatikana kwenye operesheni ya ukamataji wa magari yenye makosa mbalimbali. Magari yaliyokamatwa ni pamoja na magari 33,444,  pikipiki 795, malori 21,247,  daladala 12,197 na bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa kofia ngumu na kupakiza abiria zaidi ya mmoja maarufu kama mishikaki wakiwa ni 92.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo ijumaa Novemba 24, 2014.  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi lake linaendelea na operesheni hiyo na kuwataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Ninawataka madereva wote wazingatie sheria za usalama barabara ili kuepuka usumbufu. Tutaendelea kuwakamata wote wanaoleta usumbufu barabarani.” amesema Mambosasa na kusisitiza kwamba Jeshi hilo liko kila mahali katika jiji hili.

Kwa upande mwingine, Mambosasa amesema wamekamata magunia manne ya bangi, kete 147 za dawa za kulevya, misokoto 155 ya bangi na Lita 300 za gongo na mitambo sita ya kutengenezea kinywaji hicho haramu.

Pamoja na tukio hilo, Mambosasa amesema jeshi la polisi linawashikilia watu 140 kwa makosa mbalimbali kuanzia Novemba 10 mpaka 23. Watuhumiwa hao wahusika makosa mbalimbali yakiwamo kukutwa na dawa za kulevya, pombe haramu na bangi.

Raia wema waendelee kutoa taarifa za matukio ya uhalifu hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.” amesema Mambosasa na kutahadharisha kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wahalifu wanaokamatwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents