Mwana Mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman bin Abdulaziz ametangaza kujengwa kwa Jiji jipya ndani ya Riyadh litakaloitwa, New Murabba.
New Murabba litakuwa jiji la kisasa zaidi kuwahi kutokea kwenye uso wa Dunia ambapo litabadilisha taifa hilo ifikapo 2030, litajengwa chini ya ardhi ndani ya eneo lenye umbile la Boksi.
Video bofya HAPA
Mradi huo wa gharama za dola za Marekani trilioni moja ($1 Trillion) umeundwa ili kuimarisha ubora wa maisha, afya, ukiwa na maeneo rafiki kwa mazingira, njia za kutembea na kuendesha baiskeli, ukiwa na zaidi ya kumbi 80 za burudani na utamaduni.
Utakapo kamilika utaliongezea taifa hilo pato la dola za Marekani bilioni 48 nje ya mafuta, na kutengeneza ajira za moja kwa moja na zisizo moja kwa moja zipatazo 334,000 ifikapo 2030.
Jiji hilo ni kama yanayo onekana kwenye baadhi ya Filamu za kizungu ikiwemo ‘Avatar’ na nyinginezo ambayo majengo na mazingira yake huwa ni yakufikirika tu.
Je, utaweza kumudu gharama za kuishi kwenye mji huu..?
Imeandikwa na @fumo255 video by mitandao