Burudani

Joh Makini azungumzia collabo anayotarajia kuifanya na K.O wa Afrika Kusini

Joh Makini ameitumia vizuri fursa ya kukutana na rapper wa Afrika Kusini K.O aliyekuja Tanzania wiki hii akiwa njiani kuelekea Nairobi, Kenya.

Weusi na KO

Rapper huyo wa Weusi amesema baada ya K.O kuwasili Dar alifanikiwa kwenda naye kwenye studio ya The Industry ya Nahreel, ambapo walianza kufanya maandalizi ya mdundo lakini bado hawajarekodi wimbo ili kujiandaa zaidi uwe wimbo mkubwa.

“Tulipofikia mpaka saizi tumefikia kwenye mdundo uko tayari na sasa hivi tunajaribu kubrainstorm” Joh Makini ameiambia Bongo5. “kwasababu tumeona tukitaka kurush tu kurekodi tungeweza kurekodi lakini tunataka kufanya kitu kikubwa, kwahiyo tuko kwenye kutafuta content sababu collabo ya mimi na K.O lazima iwe ni ngoma kubwa.”

Kuna uwezekano collabo hii itakapofanywa na kukamilika ikawa ya Joh Makini amemshirikisha K.O au K.O amemshirikisha Joh kwasababu bado wako katika mazungumzo ya wimbo uwe wa nani.

“Bado tupo kwenye mazungumzo huu wimbo unaweza kuwa ni wa kwangu au unaweza kuwa ni wa kwake…bado hatujaamua unaweza kuwa ni wa mimi na yeye au unaweza kuwa ni wimbo wake kunishirikisha au mimi kumshirikisha yeye” alimaliza JOh.

Hii itakuwa ni collabo ya pili kubwa kufanywa na Joh Makini na rapper wa Afrika Kusini, baada ya ile aliyofanya na AKA ambayo bado haijatoka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents