Burudani

Julitha Kabete kuiwakilisha Tanzania mashindano ya Miss World 2017

Mrembo kutoka Tanzania Julitha Kabete, ndiyo aliyeteuliwa na kamati Miss Tanzania kwenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo wa dunia Miss World 2017 nchini China- Sanya.

Julitha amewahi kuwa Miss Africa Tanzania 2016, Climate Change Ambassador tayari amesha kabidhiwa bendera ya taifa hapo jana  kuashiria safari imeiva.

“Hi everyone, I’m honored to be representing my beautiful country Tanzania in Miss World 🌎 this year…… I am humbled to carry the Tanzanian flag higher to the world. Together with support I belive we can. Wish me Luck and prayers 🙏🏽. 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿 Watanzania wenzangu, kwa heshima na taadhima ninayo furaha kuiwakilisha nchi yangu kwenye mashindano ya kimataifa ya urembo ya dunia ‘Miss World’ Hii ni heshima kubwa sana kwangu, kwa familia yangu na kwa taifa langu. Ninshukuru Mungu kwa kwa nafasi hii ya kipekee. Kwa maombi na sapoti ya watanzania Nina hakika nitaweza kuiinua juu Bendera yetu na kuliwakilisha vyama taifa letu la Tanzania🇹🇿 ……Mungu ibariki Tanzania🙏🏼,” ameandika mrembo huyo katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Warembo kutoka nchi 120 wanatarajiwa kushiriki shindano hilo ifikapo Novemba 18 mwaka huu nchini China katika ukumbi wa Sanya City Arena. Kituo cha E! na Phoenix TV, ndiyo wataoorusha matangazo mubashara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents