Burudani

K.O na Cassper Nyovest kusindikiza show ya T.I, SA, wasouth wanadhani ni mara yake ya kwanza kutumbuiza Afrika!

Rapper T.I. anatarajia kutumbuiza nchini Afrika Kusini mwezi March.

T.I
T.I. akitumbuiza kwenye tamasha la Fiesta, 2014, Leaders Club

Atatumbuiza kwenye tamasha la Jack Daniel, Boomtown.

Cassper Nyovest na K.O watasindikiza show hiyo. Hata hivyo vyombo vingi vya habari vya nchini Afrika Kusiini vinadhani kuwa hiyo ni mara ya kwanza rapper huyo kutumbuiza barani Afrika.

“For his first time performing in Africa, he will deliver tracks from a variety of his nine studio albums,” imeandika tovuti ya IOL.

Hii ni mara ya pili T.I. anakuja Afrika. Mwaka 2014 alitumbuiza kwenye Fiesta jijini Dar es Salaam.

T.I-akitoa-burudani

Wasanii wengine watakaotumbuiza ni pampja na Mi-Casa na Mafikizolo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents