Burudani

Kabwe asema uchunguzi ufanyike ili kubaini ukweli, ni baada ya kutumbuliwa

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amesema uchunguzi wa tuhuma zilizomfanya Rais John Magufuli kumsimamisha kazi jana utabainisha ukweli wa tukio hilo.
kabwe

Alisema hayo mara baada ya Dk Magufuli kutangaza kumsimamisha kazi wakati wa uzinduzi wa Daraja la NSSF Kigamboni ambalo sasa litaitwa Daraja la Nyerere baada ya kumwita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kueleza tuhuma dhidi ya mkurugenzi.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Jumanne hii, Kabwe alisema hakuwa na taarifa za kusimamishwa kwake na kama imetokea hivyo ni sawa kwa kuwa Magufuli ni mkubwa wake.

“Nimekwambia sina la kukwambia kwa sasa lakini nimesema tu sina shida na hilo, uchunguzi ufanyike nina uhakika ukweli utajulikana tu. Lakini kama ukijulikana na ikibainika nimeonewa je, kuna fidia yoyote nitalipwa?,” alisema Kabwe.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Jumanne hii alimlaumu mkurugenzi huyo kwa mambo kadhaa ya kiutendaji ikiwemo kuongeza mkataba wa maegesho ya magari kwenye jiji na ulanguzi wa kodi za mapango kwenye stendi ya mabasi ya Ubungo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents