Habari

Kada wa CCM auwawa kwa risasi

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Bungu wilayani Kibiti, Alife Mtulia ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema mauaji hayo yamefanyika usiku wa kuamkia leo (Jumapili) katika Kijiji cha Nyambunda.

Amesema Mtulia aliuawa na watu hao alipokuwa anakwenda kuoga.Kamanda amesema mwili wa marehemu umepelekwa kituo cha afya cha Kibiti kwa uchunguzi.

Mauaji ya askari Polisi, viongozi wa Serikali za Mitaa na raia yamekuwa yakifanyika mara kwa mara katika wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani.

Jumanne wiki hii akiwasilisha bungeni bajeti ya wizara yake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba aliliambia Bunge kuwa Serikali itaanzisha mkoa mpya wa kipolisi katika wilaya za Kibiti, Rufiji, Mkuranga na Mafia ili kuimarisha ulinzi.

Chanzo: Mwananchi

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents