Habari

Kama hali hii inaanzia vyuoni ufisadi hautakwisha

Utatamani kujua chanzo cha shida na matatizo kwenye kila nchi lakini kila jambo halitokei kwa bahati mabaya ila tu lilianza sehemu na kukua na kuendelea na mwishowe ikawa tabia ya mtu.

172133209-690x450

Vitu vingi vinavyoendelea hapa nchini havijaanzia hapo, hayo ni matokeo tu ya namna tulivyokuzwa na kulelewa. Siku chache zilizopita niliweza kupata tetesi ya ubadhilifu mkubwa wa fedha za wanafunzi katika chuo kimoja hapa nchini na kukutana na habari hii;

Mtu mmoja aliweza kuripoti hivi, Kwa ufupi ni kwamba aliyekuwa rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kimoja hapa nchini jina limehifadhiwa  alishikiliwa na jeshi la polisi siku chache zilizopita baada ya kuwekewa mtego chini ya shujaa  na ambaye sasa ndio rais wa serikali ndugu Godfrey Modest aliyekuwa makamo wake hapo nyuma.

Mtego huo ulisukwa chini ya polisi kwa kuanza kufuatilia fedha iliyotolewa hivi majuzi juzi katika account ya serikari ya wanafunzi na kubaini uchotwaji wa mamilioni kwa kugushi sahihi ya mkufunzi msimamizi wa wanafunzi baada ya uchunguzi huo mfupi shujaa wetu aliambatana na askari kanzu hadi eneo alipokuwa amepanga chumba huyo mwizi wa fedha zetu, maeneo ya kigogo.

Kwa ubunifu na mkakati mzuri  wakamkuta akiwa na wenzake na kufanya ukaguzi ndani wakabaini fedha zingine zikiwa ndani zaidi ya 16m na ndipo akatiwa pingu kupelekwa anapostahili kupisha uchunguzi zaidi! Waziri wa serikari ya wanafunzi wa chuo hicho alisema “Nikiwa kama waziri wa elimu wa serikali iliyokuwa inaongozwa na jambazi huyu wa fedha za wanafunzi napenda kuwahakikishieni kuwa tumesikitishwa na ulanguzi huu wa pesa ya umma na wote walioshiriki sheria itafata mkondo wake! Kwa taarifa zaidi mtaendelea kupewa na watakieni siku njema”

Kutokana na habari hiyo nikagundua kuwa msingi wetu wa maadili unaharibiwa tangu chini hivyo mtu anaendelea kukua na kupata nyazifa za juu na kuendelea kufanya kile kile alichozoea tangu zamani.

Katika maongezi na watu wengine tuliweza kuangalia mambo kadhaa, mfano wengi tumekulia kwenye familia ambazo ukilinganisha kipato cha mzazi na maisha anayoishi haviendani kabisa. Mshahara ni mdogo ila maisha yanakuwa mazuri na hakuna anaweza kuhoji hivyo hata kizazi kinachoendelea kukua huwa hakijui mafanikio ya wazazi wao yanatoka wapi mpaka wakifika juu, ndipo wanagundua mchezo mzima.

Je tunamalije ufisadi kama ni sehemu ya maisha yetu? Tunachokiona huko juu ndicho hicho kinaendelea kwenye maisha ya watu wengi nchini kila kitu tunatafuta wapi kwa kupiga au dili hili na mimi napata nini? Kwasasa tunatofautiana tu nafasi.

Hicho ni chuo kimoja tulichoweza kugundua, je kwenye vyuo vingine kunatokea nini?

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents