Habari

Kama serikali haina majibu tunayouliza bungeni isitujibu – Mbunge Yussuf

Mbunge wa CUF Jimbo la Chambani Pemba, Yussuf Salim Hussein, ameitaka serikali kuwa wanapouliza mwaswali wakiwa bungeni kama haina majibu yakuwapa ni bora isijibu.

Hussein ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akimuuliza Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati alipouliza kuhusu swali la vifaranga milioni 21 vinavyozalishwa. Hivi ndivyo alivyouliza swali lake.

“Kwa masikitiko makubwa niiombe serikali inapokuwa haina majibu tunayouliza basi isitujibu , Swali hili nilichangia bajeti ya mwaka 2015/2016 Naibu Waziri akiwa Ole Nasha yule pale akanijibu hivi ni vifaranga vya mfano milioni 21 ndiyo vimezalishwa kwaajili ya kuwapelekea wakulima ipo kwenye bajeti ya wizara hii 2015/2016 leo serikali inaniambia kutoka 2009,2010 mpaka 2017/018 imzalisha viranga milioni 21 na kuvigawa tukisema Mh. Jenista anakuja juu ni uongo uliotukuka Mh. Kama serikali haina majibu isitujibu kwasababu tunafuatilia haya mambo sasa mimi siwezi kukubali kama serikali ina mpango huu,” alihoji Mbunge Yussuf.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents