Habari

Kamanda Sirro awataka Watanzania wasiogope waitwapo polisi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam limesema kuwa hakuna sababu woga kwa wale watu waliotajwa kwenye orodha ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa kuna miongoni mwa watu waliotajwa wamekuwa wakipiga simu kuulizia kuna nini na wengine wanawatuma ndugu zao.

“Hakuna sababu ya kuwa na woga mpaka kumtuma ndugu kwa Kamishna Siro, bali unapoitwa njoo uripoti kwa timu iliyoundwa na mkuu wa mkoa, watapeleleza mambo yote ukionekana huhusiki utaachiwa,” alisema Kamanda huyo.

Aidha kamanda huyo alisema kuwa juzi walikwenda watu wa mahotelini (wamiliki),baada ya kuhojiwa walionekana hawana jambo zito na la msingi hivyo waliachiwa huru.

Hata hivyo alisema oparesheni ya dawa ya kulevya bado inaendelea ambapo Jumatano walikamatwa watu 11 na kete 38 za dawa ya kulevya na magunia sita ya bangi.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents