Habari

Kanisa Katoliki lamlipa Tsh bil. 4 mwanaume aliyenyanyaswa kigono utotoni na Katekesta

Kanisa Katoliki Dayosisi ya Erie jimbo la Pennsylvania mjini Marekani, limemlipa fidia mwanaume mmoja aliyenyanyaswa kingono na Katekesta Kanisani hapo mwaka 2002.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail, Mwanasheria wa mwanaume huyo aliyenyanyaswa kingono, Mitchell Garabedian amesema kuwa Kanisa hilo limemlipa jana Jumanne kama fidia kutokana na kitendo hicho .

Katekesta huyo aliyemfanyia mwanaume huyo vitendo hivyo, David Poulson mnamo mwezi Januari mwaka huu, alihukumiwa miaka 14 jela kwa kosa la kulawiti mtoto mwaka 2002 na miaka 2 mingine kwa kosa la kumnyanyasa kingono mtoto mwingine wa kike kwa kumuonesha picha chafu mwaka 2010.

Hata hivyo, David Poulson (65) licha ya Kanisa hilo kumlipa muathirika bado yupo Jela, na tayari Vatican mwezi huu (Machi) imetangaza kumvua hadhi yake ya kutumikia kanisa hilo, hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Dayosisi hiyo ya Erie .

Malipo hayo, yamefanywa na Kanisa hilo kama pole kwa muathirika wa tukio hilo la unyanyasaji kingono.

Kanisa Katoliki ulimwenguni kote lipo katika vita ya kukomesha kashfa hizo zinalolichafua kanisa hilo kwa kipindi kirefu.

Mwezi Februari Mwaka huu, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis aliongoza mkutano wa kihistoria, Mjini Vatican, uliojadili jinsi ya kukabiliana na manyanyaso ya ngono dhidi ya watoto, tuhuma ambazo zimekuwa zikilitafuna kanisa kwa miongo kadhaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents