Habari

Kazi 2 zinazochukuliwa poa Bongo zinazoweza kuwapa mamilioni vijana

Kwa kadri maisha yanavyokwenda, kazi za kuajiriwa zinazidi kuwa adimu. Katika mazingira hayo, watu, hasa vijana wanatakiwa kujiajiri wao wenyewe. Lakini vipi kama huna ujuzi lakini una kipaji? Ama una ujuzi lakini umekosa ajira?

Stan Pearson Teaches SALSA

Watu wengi duniani wanatajirika sababu ya vipaji vyao. Wanasoka, waigizaji, wanamuziki, wachoraji na fani zingine wametajirika kwa kutumia vipaji vyao. Kuna sanaa au fani zingine ambazo katika nchi zilizoendelea zinawapa watu utajiri mkubwa lakini kwa Tanzania bado fursa haichangamkiwa zaidi.

Hizi ni kazi mbili ambazo zinaweza kukuingizia mamilioni.

Wazungumzaji wahamasishaji (motivational speakers)

12558828_936391469743041_453873042_n
Chris Mauki: Social, Relationship and Counselling Psychologist at UDSM: MC & Motivational speaker

Sidhani kama ‘wazungumzaji wahamasishaji’ ni tafsiri sahihi ya ‘motivational speaker’ lakini kazi yao hasa ni kufundisha watu jinsi ya kutengeneza fedha kwa njia mbalimbali, kuboresha maisha yao binafsi, kupunguza uzito, mahusiano, kutambua vipaji vyao nk.

Ushawishi wao na uwezo wa kuburudisha na kuwashawishi watu kuwa watafanikiwa, ni kitu kinachowatofautisha na wazungumzaji wengine kama vile wanasiasa. Wengi ni wataalam kwenye fani zao na wamejiajiri, huku wengine wakifanya kazi kwenye makampuni, serikali, makanisani au shuleni.

Kwa nchi zilizoendelea, motivational speakers huingiza wastani wa $90,000 kwa mwaka. Ili uweze kufanikiwa ni lazima uweze kuongoza, kuhamasisha na kuelewana na umati. Ni lazima uwe mchangamfu, mcheshi, mtu wa watu, uwezo wa kuandika na kusimulia vitu.

Kama ukijitengenezea umaarufu na ukafahamika una nafasi ya kupata fedha nyingi sana kila mwaka. Baadhi ya watu ninaowafahamu hapa Tanzania na wanaofanya kazi hii ni pamoja na Chris Mauki, Harris Kapiga, Eric Shigongo na wengine. Kuna fursa kubwa ya watu wenye uwezo wa kushawishi kupata fedha kwa kazi hii. Uzuri wa kazi hii ni kwamba unaweza kuifanya kama kitu cha ziada na kukuongezea kipato.

Uchekeshaji wima (Stand Up Comedy)

917376_199948523715748_1451429515_n
MC Pilipili

Stand Up Comedy ni kazi yenye hela za bure na nyingi kama utakuwa na uwezo wa kusimama mbele ya umati mkubwa wa watu na wakacheka. Ni fani ambayo imemtoa MC Pilipili kutoka kwenye ualimu na maisha ya kawaida Dodoma, na kuwa miongoni mwa watu maarufu Tanzania.

12918471_482251841982568_351418318_n
MC Pilipili akiwa kazini

Naweza kusema MC Pilipili ni mchekeshaji wima pekee kwa sasa Tanzania aliyevumbua fursa hiyo na kuichukulia serious kiasi cha kufanya ziara mikoani. Huko anajaza kumbi kama wasanii wa Bongo Flava na anazivunja mbavu za wengi kwa vichekesho vyake.

Hakuna mtu asiyependa kucheka, hivyo ukweli huu unaifanya fani hii kuwa na fedha za uhakika kama tu ukiwa mtu mwenye talanta hii. Kwa wenzetu kama Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini, uchekeshaji wima ni fani inayowaingia mamilioni wachekeshaji wengi. Uchekeshaji wima ndiyo uliomfanya Trevor Noah, Msouth aliyepewa shavu la kumrithi Jon Stewart kwenye kipindi maarufu Marekani cha The Daily Show. Kwa Marekani ndiyo usiseme, wachekeshaji kama Jerry Seinfield na Kevin Hart wanaingiza mamilioni ya dola kila mwaka.

Kwa mfano kwa mujibu wa Forbes, Seinfeld aliingiza dola milioni 36 katika kipindi cha June 1, 2014 na June 1, 2015 kupitia kazi zake zikiwemo uchekeshaji wima.

Muda wa kuchangamkia fursa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents