Burudani

Kazi baada ya Kazi: Vanessa Mdee ashoot video mpya

Kama unadhani Vanessa Mdee atakuwa amerelax baada ya kuachia video ya Niroge, fikiria mara mbili kwasababu ni kama ndio ameanza.

12677370_219762168384995_702153954_n

Muimbaji huyo anaendelea kuthibitisha kuwa ni miongoni mwa wasanii wa Afrika wanaojituma zaidi kwa sasa kwa kufikiria na kufanya kitu kimoja tu – kazi!

Vee Money ameingia tena location kushoot video mpya na kama yeye mwenyewe anavyosema kwenye kipande cha video alichokiweka Instagram: Just create the Art, while they’re discussing whether they like it or not create more art. Najivunia ubunifu na uchapakazi. Wewe je? #Niroge #VeeInGidi.

Hivi karibuni alikuwa nchini Nigeria na kuna uwezekano mkubwa kuwa video hiyo ikawa imefanyika huko. Kabla ya hapo alishare picha nyingine kwenye Instagram akiwa location na kuandika: Brewing something Majaaah #Niroge #VeeInGidi.”

12950279_1689872477952255_942942229_n

Vee ameendelea na maandalizi ya album yake, Money Mondays itakayotoka mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents