Burudani

Mzee Yussuf kuachia wimbo mmoja wa Hip Hop kwa ajili ya mashabiki

Mfalme wa muziki wa taarab Mzee Yussuf amesema zamani kabla hajaanza kuimba muziki wa taarab alikuwa akifanya muziki wa Hip Hop.
Mzee Yussuf

Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Mzee Yussuf amesema ukifika wakati atatoa kibao kimoja cha muziki wa Hip Hop ili kuwaburudisha mashabiki wake.

“Mimi zamani nilikuwa chini ya Ruge, nilikuwa nachana kabisa, lakini sio ile ngumu, yangu ilikuwa ina ‘ubongofleva’,” alisema Mzee Yussuf. Lakini baada ya kukaa muda mrefu ndio nikaanza kuimba taarab lakini ipo siku nitawafurahisha mashabiki wangu kwa wimbo mmoja,”

Katika hatua nyingine Mzee Yussuf amewataka mashabiki wa muziki wa taarab kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kazi zake mpya mbili ambazo zitatoka hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents