Habari

Kenyatta awakataa maofisa wapya walioteuliwa na Tume ya Uchaguzi

Chama cha Jubilee cha Rais Uhuru Kenyatta kimewakataa maofisa wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ambao wanatarajiwa kusimamia uchaguzi mpya wa Urais mwezi ujao Oktoba 17.

Uhuru Kenyatta

Chama hicho kimetoa orodha ya majina ya maofisa hao, ambao kimesema wanawafahamu kuwa wanapendelea wapinzani.

Siku moja iliyopita Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alitangaza maofisa saba watakaoongoza maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika Oktoba 17. ambapo miongoni mwa maofisa hao ni Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na msimamizi wa kituo cha Taifa cha kujumlishia matokeo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limesema “Tuna habari za kuaminika kwamba kwenye orodha ya maofisa hao kuna watu wanaofahamika wazi kuegemea upande fulani.”

Leo Rais Uhuru amekutana na viongozi wa kidini ikulu ambapo amesema tarehe iliyotangazwa inafaa ili kutovuruga kalenda ya mitihani ya taifa ambayo imepangiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Mahakama ya Juu nchini Kenya Septemba Mosi ilifuta matokeo ya Urais kwa kudai ulikuwa na dosari ambapo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 8 ambao Rais Kenyatta alitangazwa mshindi.

Katika uchaguzi wa Agosti 8, Kenyatta alitangazwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27, huku mpinzani wake Odinga akipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74.

Hivi karibuni Muungano wa National Super Alliance (NASA), ambao mgombea wake ni Raila Odinga, ulidai mabadiliko makubwa kwenye IEBC kabla ya uchaguzi mpya kufanyika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents