
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Kenyana Uganda kupitia Pamoja Bid wameadhimiria kuwa mwenyeji wa Michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (African Cup of Nations) 2027.
Rais Samia amesema nchi hizo zinawania nafasi hiyo kwa kutambua mafanikio makubwa ambayo Sekta ya Michezo imepata, hivyo kuwa wenyeji wa AFCON 2027 kutaongeza hamasa zaidi kwa ukuaji wa michezo hususan soka.
Aidha Rais Samia amesema michuano hii itachangia katika ukuaji wa utalii kwa kuwa ni mashindano ambayo hutazamwa na zaidi ya watu bilioni moja Barani Afrika na maeneo mengi duniani kwa ujumla.