Habari

Kesi ya rushwa dhidi ya Jacob Zuma kuendelea leo

Kesi ya muda mrefu ya rushwa inayomkabili Rais wa zamani wa Afrika Kusini aliyeko jela Jacob Zuma itaendelea leo kwa njia ya video, licha ya vurugu kali ambazo zimelikumba taifa hilo baada ya kufungwa jela katika kesi nyingine.

Zuma anakabiliwa na mashitaka 16 ya ulaghai na rushwa kuhusiana na ununuzi wa mwaka wa 1999 wa ndege za kivita, boti za kushika doria na vifaa vya jeshi kutoka kwa kampuni tano za kijeshi barani Ulaya wakati akiwa naibu wa rais.

Anatuhumiwa kupokea hongo kutoka kwa moja ya kampuni hizo, Thales ya Ufaransa, ambayo ilishitakiwa kwa rushwa na utakatishaji pesa.

Kesi hiyo ilianza Mei baada ya kuahirishwa na kucheleweshwa mara nyingi, wakati timu ya utetezi ya Zuma ikipambana kutaka mashitaka hayo yafutwe. Zuma mwenye umri wa miaka 79, anasisitiza hana hatia. Kampuni ya Thales pia ilikana mashitaka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents