Fahamu

Kifahamu kijiji kilichopotea Kwenye ziwa kwa miongo na chapatikana Italia (+ Video)

Kazi ya ukarabati kwenye eneo linalovutia utalii zimefichua mabaki ya kijiji ambacho kilipotea chini ya maji miongo kadhaa iliyopita. Ziwa Resia, lililopo katika eneo la kaskazini mwa nchi ya Italia ni maarufu sana kwa kuwa na kanisa lenye mnara mrefu.

Eneo hili la kihistoria hata limewafanya watu waandike kitabu kulihusu na kuijfanya Netflix kutengeneza filamu ya vichekesho kulihusu.

Lakini kutokana na kupotea kwa maji katika ziwa hilo , wakazi hatimaye wameweza kugundua, Curon, kijiji ambacho wakati mmoja kilikuwa ni makazi ya mamia ya watu kabla ya kufurika ili kutengeneza kiwanda cha umeme

ziwa

Ziwa Resia – au Reschensee kama linavyofahamika kwa kijerumani -liko katika eneo la Kusini mwa Tyrol, katika jimbo la Alpine lililoko kwenye mipaka baina ya nchi za Austria na Switzerland.

Picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha kuta ambazo kwa kawaida zingekuwa chini ya ziwa, zilikuwa karibu na mnara unaotambuliwa wa kanisa lililojengwa karne ya 14.

 

Luisa Azzolini, ambaye anatoka katika eneo hilo, alituma ujumbe wa Twitter kwamba ilikuwa ni hisia ya ajabu” kuamka na kutembea kati kati ya vifusi vya kijiji cha zamani.

kijiji

Kijiji cha Curon kilipotea ndani ya maji mwaka 1950 wakati mamlaka zilipoamua kujenga bwawa na kuunganisha maziwa mawili yaliyokuwa karibu – licha ya wakazi wake kupinga ujenzi huo.

Zaidi ya nyumba 160 zilivunjwa, na wakazi wa kijiji cha Curon wakasambaratishwa-ingawa baadhi waliamua kubakia katika kijiji kipya kilichobuniwa kwa ajili yao karibu na eneo hilo.

kijiji

Siku hizi, ziwa hilo ni maarufu kwa wanaokwea milima nyakati za kiangazi, huku wageni wakija kutembea kwenye sakafu ya barafu iliyoganda kufikia kilele cha mnara wa kanisa la zamani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents