Habari

Kikongwe wa miaka 74 akutwa na mabaki ya mwili wa mumewe uwanja wa ndege

Polisi katika uwanja wa ndege wa Munich nchini Ujerumani wamepigwa na mshangao mkubwa wakati wakichunguza sanduku la mbao lililokuwa linasafirishwa na abiria mmoja kikongwe mwenye umri wa miaka 74 ambalo waligundua kuwa lina mifupa ya mume wa mama huyo, maafisa wamesema hapo jana siku ya Jumanne.

Woman with husband's bones gets close look at Munich Airport ...

Maafisa wa forodha, daktari na waendesha mashitaka waliitwa, na kugundua kuwa hakuna uhalifu uliofanyika, shirika la habari la Ujerumani dpa limeripoti.

Baada ya kumhoji mwanamke huyo na mwanae wa kike mwenye umri wa miaka 52, polisi iligundua kuwa wanawake hao wawili walikuwa safarini kutoka Ugiriki kwenda katika nchi walikozaliwa ya Armenia kupitia Munich na Kiev.

Polisi wamesema Mama huyo alisema mume wake alifariki mwaka 2008 na alizikwa mjini Thessaloniki, Ugiriki na kwamba yeye na mtoto wake wa kike waliamua kurejesha mabaki hayo nyumbani nchini Armenia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents