Burudani
Kim Kardashian aitembelea Ivory Coast
Mwaka huu mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan umekuwa na bahati ya kutembelewa na mastaa wa Marekani ambapo mwanzoni kabisa mwa mwezi huu Chris Brown na Rihanna walikuwa huko kuhudhuria tuzo za Kora. Na sasa mrembo anayezungumzwa zaidi kwenye internet, Kim Kardashian ameenda kutalii kwenye mji huo. Kim alithibitisha taarifa hiyo kupitia Twitter kwa kuandika:
Amekwenda huko kwenye hafla ya uzinduzi wa simcard ya Ma Life ya mtandao wa simu wa Orange itakayofanyika leo jioni.
Kabla ya kwenda nchini humo Kim na mpenzi wake Kanye West ambao hivi karibuni walitangaza kutarajia mtoto walikuwa wote jijini Paris.