Burudani

Kim Kardashian na Kanye West waonesha picha hii ya familia kusherehekea Pasaka

Tangu alazwe na hospitali na kutoka mwishoni mwa mwaka jana, Kanye West amekuwa mkimya na kipaumbele pekee katika maisha yake sasa ni familia.

Mke wake Kim Kardashian ambaye naye anaendelea kurudi katika hali ya kawaida tangu aporwe mali mbele ya mtutu wa bunduki October mwaka jana huko Paris, Ufaransa, ndiye amekuwa akiwapa mashabiki wao walau fursa ya kumuona Kanye kupitia picha anazoweka kwenye mitandao ya kijamii.

Kama familia zingine duniani, Kanye na Kim wamesherehekea pamoja sikukuu ya Pasaka Jumapili hii. Kupitia Instagram, Kim ameweka picha yao pamoja na watoto wao, North na Saint.

Staa huyo wa Keeping Up with The Kardashians, amepost pia picha ya binti yake North akicheza na watoto wenzake kwenye sikukuu hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents