Michezo

Kinda wa miaka 14 Man United aweka historia, awa wa kwanza kucheza UEFA kwa umri wake akiikabili Valencia

Timu ya vijana waliyo na umri chini ya miaka 19 wa Manchester United ilifanikiwa kusonga mbele hatua ya makundi baada ya kuwafunga Valencia  jumla ya mabao 2 – 1 siku ya hii leo siku ya Jumatano kwenye michuano ya ‘UEFA Youth League’ huku kijana mwenye umri mdogo zaidi, Shola Shoretire akiandika historia ya kushiriki.

Image result for Shola Shoretire UEFA Youth League

Mashetani hao wekundu waliingia kwenye mechi hiyo huku wakiwa wamefanikiwa kushinda jumla ya michezo minne na sare moja na kuongoza Group H kwakuwa na pointi 16 wakifuatiwa na Juventus wenye alama 10.

 

Shola Shoretire ameandika historia hiyo kwakuwa mchezaji wa kwanza kwenye michuano hiyo ya vijana ‘UEFA Youth League’ kuwa na umri mdogo zaidi, akiwa na miaka 14 na siku 314. Kinda huyo aliingia dakika ya 74, na kutengeneza historia yake.

Mbali na matokeo hayo wakubwa zao, Manchester United nao watakuwa na kibarua cha kuwakabili Valencia siku wa leo huku ikiwa tayari imeshakata tiketi ya kufuzu hatua ya makundi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents