Burudani

Kingwendu kugombea ubunge mwaka 2015!!

Msanii wa filamu za kuchekesha nchini, Rashid Mwinshehe maarufu kama Kingwendu amesema yupo katika mipango ya kuwania nafasi ya ubunge wakati wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika 2015.

Kingwendu-532

Akizungumza na mtandao wa filamucentral, Kingwendu amesema kuhusu jimbo na chama atakachokitumia kutafuta nafasi hiyo bado hawezi kuviweka wazi kwa sasa kwakuwa yupo kwenye mazungumzo na washauri wake.

“Nimejipanga vya kutosha kuingia bungeni na niko kwenye mikakati mikubwa na washauri wangu wa mambo ya siasa wanaendelea kunipika, ili niive lakini habari ndio hiyo naomba watanzania waniombee tu ili nikawawakilishe,” aliuambia mtandao huo.

“Kwa sasa sitaki kuweka wazi kuhusu chama nitakachoingia nacho bungeni na jimbo lake, lakini vuguvugu za uchaguzi zikianza tu, nitaweka wazi lakini nitaingia kwa chama kinachopendwa sana na wananchi na jimbo nitakalogombae ni hapa hapa mjini Dar,” aliongeza.

Source: filamucentral

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents