Habari

Kisutu: Mahakama haina mamlaka kuondoa mashtaka yanayomkabili Dk. Ringo na wenzake

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema haina mamlaka ya kuyaondoa mashtaka ya utakatishaji fedha wa USD Milioni 3.7 katika kesi inayowakabili vigogo wa Kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms.

Vigogo hao ambao ni washatakiwa ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Wakili maarufu Ringo Tenga, Mhandisi Mkuu wa kampuni hiyo, Hafidhi Shamte , Mfanya biashara na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Odeny Chacha na kampuni ya Six Telecoms Limited.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu , Victoria Nongwa ambapo amesema uamuzi huo unatokana na hoja za upande wa utetezi kuwa kuna baadhi ya mashtaka yana upungufu kisheria.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Victoria alisema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kufanya lolote katika kesi hiyo hadi upelelezi utakapo kamilika au kibali kitakapo tolewa na DPP kuhusu kesi hiyo kusikilizwa hapo.

“Hivyo washatakiwa mtaendelea kubaki rumande hadi upelelezi utakapo kamilika naahirisha kesi hadi Disemba 12 mwaka huu.”

Washtakiwa hao wanadaiwa kuisababishia TCRA hasara ya USD 3,736,861 sawa na Tsh. Bilioni 8.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents