Habari

Kitu kimoja unachotakiwa kukisema kwenye barua ya kuomba kazi

Je kuna kitu unaweza kukisema kwenye barua ya kuomba kazi na kikakuhakikishia wewe kutimiza malengo yako na kukupelekea kuitwa kwenye usaili?

yolanda-spivey_black-woman-pretends-to-be-white-to-get-job1

Barua ya kuomba kazi inaongelea kwa kifupi kuhusu wasifu wako na kukujumuisha kama mtu anayehitajika kwenye kazi furani.

Ni sehemu pekee ya kuonyesha unahitaji hiyo nafasi ya kazi na kutengeneza uhusiano wako na mwajiri mtarajiwa. kuonyesha kwamba unahitaji kazi hiyo kwenye barua ni muhimu sana, na kuna jambo moja linalokuhakikishia utaitwa kwenye usaili.

Omba kukutana na Mwajili au Mtu anayefanya Usaili.

Je waujua usemi unaosema, ‘Ombeni nanyi mtapewa’? Ni kweli. Linaweza kuwa jambo la kawaida na ushauri wa kawaida bali ni mara ngapi umeandika barua ya kuomba kazi bila kuomba kufanyiwa usaili? wakati ni rahisi kufanya!

Wakati unamalizia kuandika barua yako, kitu unachotakiwa kukifanya ni kumuuliza mwajiri kuhusu kukwita kwenye usaili. Utafiti unaonyesha watu wanaoandika kwenye barua na kuomba kufanyiwa usaili wana nafasi zaidi ya kuitwa kuliko ukinyamaza kimya.

Unapomalizia barua yako kama ni Kiswahili

Nimevutiwa na nafasi ya kuwa Meneja Mauzo wa kampuni yenu na ningependa kupata nafasi ya kukutana nawe ana kwa ana ili niweze kuongelea uzoefu wangu na mchango wangu ninaoweza kuutoa kwa ajili ya nafasi hiyo. Tafadhali unaweza kunipigia kwenye simu namba +255xxxxxxx na kunipangia lini unaweza nifanyia  usaili kulingana na wakati na nafasi uliyonayo kukutana nami.

Kuna namna nyingi unazoweza kuomba kuitwa kwenye usaili wakati ukiandika barua ya kuomba kazi, hivyo jifunze zaidi na uongeze nafasi yako ya kuitwa kwenye usaili.

 

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents