Michezo

Klabu ya soka ya AC Milan yapigwa STOP kushiriki michuano ya Europa League barani Ulaya

Klabu ya soka ya AC Milan imepigwa adhabu ya mwaka mmoja ya kutoshiriki michuano ya Europa League msimu ujao.

AC Milan iliyomaliza nafasi ya 5 kwenye ligi ya soka Italia, Serie A imekumbana na kifungo hicho kutoka kwa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo baada ya kuvunja sheria ya ‘Financial Fair Play’.

Kwa kifungo hicho, nafasi ya AC Milan itachukuliwa moja kwa moja na AS Roma, Huku Torino iliyomaliza katika nafasi ya 7 kwenye Ligi ya Serie A msimu uliopita itaingia kwenye mechi za kufuzu ili kutinga hatua ya makundi.

Hata hivyo adhabu hiyo imetoka baada ya AC Milan kufanikiwa kukata rufaa ya kifungo cha miaka miwili, Wachopewa awali na UEFA msimu wa majira ya joto uliopita baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja sheria ya hiyo ya ‘Financial Fair Play’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents