Kocha wa Mamelodi Yanga inamuumiza Kichwa
Wakati klabu ya Yanga wakiendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa robo fainali wa klabu Bingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kocha mkuu wa mabingwa hao wa Afrika Kusini Rulani Mokwena amesisitiza kuwa wanatakiwa kuwa makini sana juu ya mchezo huo, katokana na mabadiliko makubwa ya kiuchezaji ndani ya kikosi hicho.
Mokwena ameongeza kuwa ubora wa wachezaji wa Young Africans na wale Mamelodi Sundowns utakuwa na nguvu kubwa ya kuamua matokeo ya Mchezo huo utapigwa Jumamosi Machi 30, 2024 katika uwanja wa Benjamini Mkapa saa 3:00 Usiku.
Mokwena amesema timu yake imejiandaa kupata Ushindi mbele ya Young Africans, lakini tahadhari yao nyingine ukiacha mastaa wenye uzoefu ni uwepo wa Kocha Gamondi ambaye aliwahi kuwa Kocha wa Mamelodi Sundowns halo nyuma.
“Tunahitaji kushinda tunajipanga kufanya hivyo hatutaangalia ukubwa wa jina letu tunataka ubora uamue mchezo haitakuwa mchezo rahisi kwa pande zote mbili tunawaheshimu Young Africans chini ya Kocha anayeijua Mamelodi” anasema Mokwena.
“Sisi tunajipanga kukutana na Young Africans bila kuangalia kuna mchezaji gani yupo au hayupo tunajiandaa kukutana na Young Africans iliyo kamili na kwa ubora wao” alisema Mokwena Kocha wa Mamelodi Sundowns.
Imeandikwa na Mbanga B.