HabariSiasa

Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary atua Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Mhe. Péter Szijjártó amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ziara ya rasmi ya siku mbili tarehe 27 na 28 Machi 2024.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa JNIA alipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Said Shaib Mussa.

Wengine walioshiriki katika mapokezi hayo ni Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Swahiba Mndeme; Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Gerald Mbwafu pamoja na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Hungary mwenye makazi yake nchini Ujerumani, Bi. Angela Ngailo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents