Michezo

Hatutacheza kwa hofu, watatuona vizuri – Dickson Job

Beki wa Klabu ya Yanga Dickson Job amesema wanaifahamu vizuri Mamelodi Sundowns na wapo tayari kwa ajili ya kuvaana nao Jumamosi ijayo. Job ambaye ni nahodha msaidizi wa timu hiyo amesema wanafahamu ubora wa Mamelodi, lakini kwao wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanakabiliana nao ndani ya Uwanja.

“Mazoezi tunayofanya yatakwenda kutoa picha halisi tutawezaje kushinda na kuwazuia wapinzani wetu, kwa kutumia ubora wetu na kikosi kipana tulichonacho, tumevuka hatua ngumu nyingi na kushinda sehemu ambayo wengi hawakutupa nafasi.”

“Jambo zuri tuna kocha anayeijua Mamelodi na ni lazima atatupa mbinu ya kuwamaliza kwani anawafahamu vizuri, kwa kweli hatutacheza kwa hofu ya kuangalia jina la mchezaji au nchi kwani tunachotafuta ni ushindi utaotupa wepesi wa kutinga nusu fainali tunaamini tuna uwezo mkubwa wa kushinda mechi huu” alisema Dickson Job.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents