Kocha wa Simba Pablo Franco mkali wa Real Madrid atua Tanzania

Kocha mpya wa Mabingwa wa Nchi Simba SC Pablo Franco amewasili nchini tayari kwa kuanza rasmi kibarua chake cha kukinoa kikosi hiko cha Miamba ya soka Afrika Mashariki na Kati.

Mkali huyo wa Real Madrid atakuwa na kazi kubwa ya kurudisha makali ya Simba ambayo kwenye siku za hivi karibu yakionekana kama vile yanapotea.

Lakini pia Franco atakuwa na kibarua kizito cha kuutetea Uningwa wa ligi kuu ambao watangulizi wake wameutetea kwa miaka minne mfululizo.

Atakuwa na kazi kubwa hasa ukizingatia wale anaoshindana nao kwa maana ya Yanga na baadhi ya timu nyingine za ligi kuu kuwa katika viwango bora zaidi msimu huu ukiilinganisha na Simba ambayo inayoonekana kama kusua sua hivi.

Licha ya CV kubwa aliyonayo Mhispania huyo lakini haonyeshi kuwa na uzoefu mkubwa na soka la Afrika ukilinganisha na watangulizi wake ndani ya Simba na hivyo Uongozi na Mashabiki watalazimika kumpa muda wa kutosha ili kuweza kuja kufanya makubwa.

Related Articles

Back to top button