Kuapishwa kwa Biden, Majimbo ya Marekani chini ya hali ya tahadhari

Majimbo yote 50 ya Marekani yamewekwa katika hali ya tahadhari kutokana na uwezekano wa maandamno ya ghasia wikendi hii, kabla ya kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden siku ya Jumatano.

Maelfu ya maafisa wa kikosi cha ulinzi a kitaifa wamesambazwa ili kuimrisha usalama

Vikosi vya ulinzi wa kitaifa vimetumwa kwa wingi katika mji wa Wshington DC ili kuzuia kuzuka kwa ghasia mbaya za wiki iliopita.

Shirika la FBI limeonya kwamba huenda kukatokea maandamano ya ghasia yatakayotekelezwa na wafuasi wa rais Trump katika mjaimbo yote 50.

Wakati huohuo, kundi la Biden limeweka mipango kufutilia mbali baadhi ya sera zilizoweka na rais Trump.

Muda mfupi baada ya Joe Biden kuingia katika Ikulu ya Whitehouse , ataanza kubadili baadhi ya maagizo yaliowekwa na Trump kama njia ya kuonesha tofauti kati ya utawala unaoondoka na unaoingia , kulingana na barua ilioonekana na vyombo vya habari vya Marekani.

Atairudisha Marekani katika makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi – ikiwa ni makubaliano ya kupunguza gesi chafu.

Atabadili marufuku ya kusafiri kwa baadhi ya mataifa yalio na Waislamu wengi.

Atahakikisha kuwa uvaaji wa barakoa ni lazima katika majimbo yote na wakati raia wa taifa hilo wanaposafiri kutoka jimbo moja hadi jingine

Ijapokuwa rais mteule Joe Biden kama rais Trump atalazimika kutumia uwezo wake kama rais kama njia ya kulivuka bunge katika baadhi ya masuala , mpango wake wa kuinua uchumi wa $1.9tn (£1.4tn) uliotangazwa mapema wiki hii utalazimika kuidhinishwa na wabunge ,mbali na muswada wa marekebisho ya uhamiaji .

Eneo kubwa la Washington DC litafungwa kabla ya sherehe ya kuapishwa kwa Joe Biden huku maelfu ya maafisa wa kikosi cha ulinzi wa kitaifa wakisambazwa kila mahali.

Barabara nyingi – nyengine zikiwa mbali na majengo ya Bunge , eneo la ghasia mbaya za tarehe sita Januari – yamezuiwa na vizuizi na ua wa chuma.Maeneo mengi yamewekewa vizuizi

Eneo la National Mall ambalo hushuhudia maelfu ya watu kwa sherehe hiyo ya kuapishwa kwa marais limefungwa kutokana na ombi la kikosi cha upepelezi – kitengo kinachomlinda rais.

Kundi la bwana Biden tayari limewataka Wamarekani kutosafiri hadi mji mkuu wa taifa hilo kwa sherehe hiyo kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Maafisa wamesema kwamba raia wanapaswa kutazama sherehe hiyo kutoka majumbani.

Related Articles

Back to top button
Close