Habari

Kulipa kodi ni uzalendo – Waziri Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa kulipa kodi uzalendo huku akisema mipango iliyojiwekea na serikali haiwezi ikafanikiwa endapo nchi itazembea katika ukusanyaji kodi na mapato ya serikali.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo jana Bungeni Mjini Dodoma wakati akisoma hotuba ya kuhairisha mkutano wa 7 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Ni ukweli usiopingika mipango tuliyojiwekea haiwezi ikafanikiwa endapo tukizembea kukusanya kodi na mapato ya serikali hivyo serikali itaendelea kulinda vyanzo vya mapato, kuimarisha ukusanyaji wa mapato wenyewe kudhibiti biashara za magendo kuimiza matumizi ya mashine za Kielekroniki katika kukusanya mapato na kudhibiti katika ukadiliaji wa ushuru wa forodha. Kulipa kodi ni uzalendo tuwahamasishe,” alisema Waziri Mkuu.

“Mheshimiwa Spika kulipa kodi ni uzalendo na tuwahimize wananchi wenzetu waone fahari sehemu ya mafanikio ya nchi yetu kulipa kodi na kuwafichua wasiolipa kodi, ahadi yetu ni kuikusanya kila senti itakayo kusanywa ili itekeleze jukumu lililo kusudiwa.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents