Burudani

Kuna raha yake msanii kwenda kwenye tamasha na mke wako – Hamza Kalala

Msanii mkongwe wa muziki wa bendi, Hamza Kalala amefunguka kwa kusema kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii ambao walikuwa wanazunguka kwenye matamasha akiwa na mke zao.

Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo ‘Ngondoigwa’ amedai kuna raha yake kwa msanii kuzunguka na mke kwenye matamasha.

“Mimi nilikua naenda na mke wangu sehemu zote nazofanya tamasha la muziki, Kuna raha yake kwenda na mkeo bwana,” Hanza Kalala alikiambia kipindi cha Joto La Asubuhi cha EFM.

Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii wakongwe wa muziki waliopata mafanikio makubwa katika kazi yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents