Burudani

Fid Q adai pongezi anazopewa na watu wazito zinamuongezea ‘headache’

Unaposifiwa kwa kazi nzuri unayoifanya unajisikiaje? Furaha ni hisia unayoisikia bila shaka, na kwa wengi sifa huwapa moyo wa kujituma zaidi. Lakini, sifa pia huweza kukupa wajibu mwingine wa kuhakikisha huwaangushi waliokusifia.

Na Fareed ‘Fid Q’ Kubanda, ni mmoja wa watu ambao mwezi huu wamezioga sifa, tena kutoka kwa watu wazito. Naibu Waziri wa Afya, Hamis Kingwangalla na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, wote wamemsifia mwezi huu kwa umaridadi wake kwenye hip hop.

Kama haitoshi, Nay wa Mitego alidai kuwa huchukia anaposikia watu wakimfananisha Fid Q na rapper mwingine, huku mtayarishaji mkongwe wa muziki, P-Funk akikiri kuwa, Fid kwa sasa ni mcee namba moja duniani.

Pongezi hizi Fid anazichukuliaje?

“Kweli hizi appreciation nazichukulia kama mzigo wa mwiba,” Fid ameiambia Bongo5.

“Zinaniongezea headache kiukweli, zinanifanya nijisikie kwamba kwahiyo sasa hivi nina masikio ya watu wengi ambao wana heshima kwenye jamii. Na wao pia wamechukua jukumu la kuikumbusha au kuiaminisha jamii au kuiamsha juu ya sanaa yangu. Kiukweli huo ni mzigo wa mwimba, naposema hivyo namaanisha kwamba sasa nahitaji kuendelea kufanya kama ambavyo nilikuwa nafanya siku zote au zaidi ya vile,” amesisitiza Ngosha.

Amekumbusha pia kuwa alipotoa album yake ya pili, Propaganda, aliwahi kukutana na Profesa Issa Shivji pamoja Mzee Walter Bgoya mwanzilishi wa Mkuki na Nyota na Publishers (kampuni kongwe ya uchapishaji vitabu nchini), waliomuambia kuwa ana uprofesa ndani yake.

Walimweleza kuwa wimbo wake mmoja anaweza kuandika vitu ambavyo wataandika kwenye vitabu vitatu.

“Wewe unaweza kuviweka kwenye 16 bars, unawezaje. Mimi kama Profesa Shivji siwezi,” Fid anawanukuu wazee hao. Fid anadai kuwa amekuwa akipokea pongezi hizo kwa muda lakini sasa nyingi zimekuwa zikitolewa hadharani na mashabiki wanaziona wenyewe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents