Burudani

Labda ni wakati wa kumwacha Harmonize awe ‘Harmonize’

Alhamis hii, Dully Sykes na Harmonize waliachia single yao mpya iitwayo, Inde yenye kila dalili za kuwa wimbo mkubwa Tanzania.

Na pengine unaweza kuwa wimbo wa kwanza kati ya mingi sana ambayo Dully Sykes ametoa katika miaka ya hivi karibuni kufanikiwa. Kwamba unaweza kuwa wimbo utakaovunja mkosi wa miaka kadhaa wa Dully katika kupata hit single! Mrejesho hadi sasa unaonekana kuwa Dully amewafurahisha wengi.

Lakini pamoja na uzuri wa wimbo huo, mashabiki wa Diamond wameonekana kuchoshwa na jinsi Harmonize anavyosikika kama bosi wake kwenye nyimbo anazofanya. Wanaendelea kusisitiza kuwa Harmo ni Diamond ‘number two.’
Hii si mara ya kwanza kwa Harmonize kushutumiwa kuimba kama Diamond na hata kwenye wimbo wake wa hivi karibuni ‘Matatizo’ muimbaji huyo anasikika akifanana kwa kiasi kikubwa na uimbaji wa Chibu.

Lisemwalo lipo na kama linasemwa na watu wengi kiasi hicho na wengi wao wakiwa mashabiki wake mwenyewe, basi kuna tatizo. Lakini vipi kama hivyo ndivyo Harmonize anavyosound? Vipi kama sauti yake na Diamond zinafanana tu naturally na kwamba imekuwa kama ‘coincidence’ kuwa amesainishwa kwenye label ya Dangote, WCB.

13827271_1416624831698154_1059966669_n

I mean tunaweza tukamweka mtoto wa watu kwenye kitimoto kuwa anamwiga bosi wake kumbe ndivyo alivyo na kumshutumu anakopi ni kumuonea tu. Vipi kama huyo ndio Harmonize? Labda ni wakati sasa wa kumwacha Harmonize awe Harmonize na kuacha kulazimisha kuwa Harmonize ni Diamond!

After all the kid is talented na nyimbo zake tunazipenda. Pia yeye si msanii wa kwanza kufanana uimbaji au sauti na mtu mwingine. Ona jinsi ambavyo Desiigner anavyosound vile vile kama Future. Ni kitu kinachowachanganya mashabiki lakini ukweli ni kwamba Desiigner ndivyo alivyo hata ukimwahidi umpe dola milioni 10 aimbe tofauti hatoichukua sababu atasound vile vile – kama Future.

Sikia jinsi Bill Nas anavyosound kama Godzilla wakati fulani. Yeye mwenyewe Bill anasema anasikika tofauti na kwamba Godzilla si msanii aliyemuinspire hata kidogo. Wakati mwingine makoo hutokea kufanana tu na kamwe wahusika hawana jinsi ya kuukwepa ukweli huo – si rahisi kama unavyodhani.

Labda cha msingi ni kumuonya Harmonize aepuke sana kufuata kila kitu anachofanya bosi wake kama vile uchezaji kwenye video, utikisaji wa kichwa na mabega na hata uvaaji sababu kama inawakera mashabiki wake mwenyewe, si kitu kizuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents