Burudani

Lava Lava hakutengemea hili kutoka kwa Hamisa Mobetto, ‘Alishanifuata akaniambia’

Msanii wa Bongo Flava, Lava Lava amesema mwanamitindo Hamisa Mobetto ni shabiki yake namba moja na mwanzo kabisa ni kitu ambacho hakukitegemea.

Kauli ya muimbaji huyo inakuja mara baada ya Hamisa kuposti clip ya video Instagram huku akiimba wimbo wa Lava Lava uitwao Atatulia.

Lava Lava katika mahojiano na The Playlist ya Times Fm amesema katika jitihada zake za kutoka kimuziki Hamisa Mobetto amekuwa na mchango pia.

“Nashukuru sana nyimbo zangu kina dada huwa wanazipokea kwa mikono miwili, hajalishi wapo kwenye hali gani,” amesema.

“Katika watu waliowahi kunionyesha ile love ambayo sikuwahi kuitegemea wala kuwaza ni huyo Hamisa Mobetto kwa utokaji wangu, alishanifuata akaniambia nakukubali sana, kwa hiyo ni sabaiki yangu namba moja,” amesisitiza Lava Lava.

Lava Lava kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Gundu. Pia utakumbuka hivi karibuni Hamisa Mobetto ameonyesha nia ya kutaka kuingia katika muziki mara baada ya kuachia kipande cha wimbo wake mtandaoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents