Burudani

RIP E-Sir: Leo ni miaka 10 tangu rapper huyo wa Kenya afariki kwa ajali

Leo ni miaka 10 tangu rapper wa Kenya anayeaminika kuwa na mchango mkubwa katika kukubalika kwa muziki wa kizazi kipya wa Kenya, Issah Mmari, aka E-Sir afariki dunia.

esir

Alizaliwa May 20, 1981 katka kitongoji cha California, jijini Nairobi. Alikuwa chini ya label ya Ogopa DJs na anakumbukwa kama rapper mahiri aliyeimba nyimbo kwa Kiswahili zilizohit. Mpaka leo hii E-Sir anatambulika kama miongoni mwa rappers bora kabisa kuwahi kutokea kwenye hip hop ya Kenya.

E-Sir alifariki kwenye ajali ya gari March 16, 2003, akiwa na mwenzake kwenye label ya Ogopa, Nameless. Alikuwa akielekea kwenye concert mjini Nakuru kupromote albam yake.

Mashabiki wake walishtushwa mno na taarifa za kifo chake kwani kilimchukua katika kipindi ambacho ndio alianza kufanikiwa. Alikuwa ameacha hits kibao “Mos Mos,” “Boomba Train,” “Hamunitishi” na “Leo ni Leo.” Wimbo uliotoka baada ya kifo chake ni ule aliofanya na Nameless “Maisha”

http://www.youtube.com/watch?v=y7t-YeP2IMc

E-Sir alifariki akiwa na tuzo kadhaa kama ya Kora mwaka 2003, Best East African Artist na ya tuzo za Kili Best East African Album (“Nimefika”)

Mastaa kibao wa Kenya leo wamemkumbuka ambapo Wahu ameandika kupitia Facebook, “10 years ago we lost a very important member of the Kenyan Music industry…and today, on what would have been his 32nd b-day, i want you guys to help me celebrate the life that he lived, and the legend that he left behind. R.I.P E-Sir…you continue to stay alive in the music that you left us.”

Naye Avril ametweet: #Esir how I wish I met you..my producer is always talking about you when we have our father-daughter moments..almost feels like I know you.

Mzazi Willy M. Tuva ‏mtangazaji wa Radio Citizen na Citizen TV ametweet: Siku ya leo tunasherehekea maisha ya E-SIR. Take a moment of silence na umkumbuke marehemu E-SIR | R.I.P

Collo_KING: 16/3/13 Issah Mmari. In Loving Memory of you. G.O.A.T. We miss you.

BIGPIN: TENTH ANNIVERSARY MY BIGGER NIKKA #esir will forever rep u…till the end…mad luv and respect…

Octopizzo: R.I.P to E_sir its been 10 years Since you passed on 16/3/2003 and its been 10 years Till I lost My mum Too so as I remember you I remember My mum too we Miss you Guys and how I just wished that R.I.P stands for R(eturn I(f P(ossible. R.I.P E_SIR R.I.P MUM I still Represent You in Spirit. Moment of Silence.

AY: R.I.P E-Sir,10 years nw..Umetuachia muziki mzuri sana na bado utakaa miaka mingi mbele #Kenya#OgopaDjs #BoombaTrain

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents