Burudani

Lil wayne ‘aitukana’ Marekani kwa namna yake! Aikanyaga-kanyaga bendera ya taifa hilo huku aki-Rap kwa swagg kama anatembea juu ya kapeti! (Video)

Wa Marekani walio wengi wamesikitishwa na kitendo alichokifanya Lil Wayne baada ya kuikosea heshima nchi yao ya Marekani, kwa kuamua kuikanyaga kanyaga bendera ya nchi hiyo kwa makusudi kama vile yuko juu ya kapeti la kawaida ama tambaa la deki.

lil wayne akikanyaga bendera

Tukio hilo lilitokea wikendi hii wakati Weezy alipokuwa ana shoot video yake mpya “God Bless Amerika” huko Orleans, Marekani.

Ilianza hivi, wakati video shoot inaendelea Wayne alianza kurap mbele ya bendera kubwa ya Marekani ambayo baada ya muda ilitupwa chini na rais huyo wa Young Money hakusita kuanza kuikanyaga kwa swagg huku akiendelea kurap.

Baadhi ya mashahiri ambayo pia ni controversial ya wimbo huo yanasema “My country ’tis of thee / Sweet land of kill ’em all and let ’em die / God bless Amerika / This ole’ godless Amerika.”

Tazama video clip ya Lil Wayne akiikanyaga bendera ya nchi yake

http://youtu.be/B8P6ZuUwX5k

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents