Linah afunika New Maisha Club
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Linah Sanga, juzi katika usiku wa Valentine Day, ametoa rasmi albam yake kwa mashabiki wake wote katika tamasha alilolifanya New Maisha Club.
Akiongea na Bongo5 Mlimani City, alisema kwamba ulikuwa ni uzinduzi wa albamu zao, lakini zilichelewa kidogo kuingia sokoni kutokana na sababu za hapa na pale, lakini usiku huo wa juzi ndiyo albamu yake na mwimbaji mwenzie Barnaba aliyezindua yake Mwanza, zinaingia sokoni rasmi.
Albamu hiyo inayokwenda kwa jina la Atatamani,ina nyimbo kumi zilizoshiba, na ana uhakika itafanya vizuri katika soko la muziki kwani ni alivyovipangilia, kulingana na soko husika na mahitaji ya mashabiki wake.
Linah akiwa stejini akiimba baadhi ya nyimbo zake
Mwanamuziki Ditto, alikuwepo kushoo love kwa msanii mwenzake toka Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), huku na yeye anasubiri siku mbili tatu kutinga sokoni na yake.
Matalum ndani ya nyumba
Kijana anayekuja kwa kasi toka THT, Beka, akikonga vizuri nyoyo za mashabiki wake,
Designer akiperform ‘Warembo wananipenda miye….’
Warembo wakishoo love na Bongo5.
Back up haoooo
Wapendanao nao waliingia kati kuonyesha manjonjo