Habari

Lipumba amvua Maalim Seif Ukatibu Mkuu wa CUF na kumpa Magdalena Sakaya

Baraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) Jumanne hii limemvua, Maalim Seif nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Chama hicho na nafasi hiyo kukaimiwa Bi. Magdalena Hamis Sakaya.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CUF Taifa, anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa Baraza hilo limefikia uamuzi huo kutokana na sababu mbalimbali ambapo moja wapo ni Maalim Seif kutofika ofisini na kutohudhuria kwenye vikao vya chama vinavyotambulia kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

“Miongoni mwa ajenda tulizo zijadili ni kuthibitisha wakurugenzi na manaibu wakurugenzi, kupitisha jina la wagombea Ubunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kujaza nafasi za wajumbe wa Baraza Kuu zilizokuwa wazi, kuunda Bodi ya wadhamini, kuunda kamati ya maadili, taarifa ya fedha, taarifa ya kesi na taarifa ya hali ya kisiasa,”.

Pia Prof. Lipumba ametangaza majina matatu ya Wagombea Ubunge Bunge la Afrika Mashariki kupitia majina yaliyoteuliwa na kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kilichokaa Machi 25 na 26 mwaka huu.

Majina matatu yaliyoteuliwa na Baraza kuu la uongozi la Uongozi ni, Sonia Magogo, Mohammed Habib Mnyaa na Thomas Malima mmoja kati yao akitoa serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mbali na hayo, Lipumba amemtangaza rasmi Bw. Abdul Kambaya kuwa Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma ambapo hapo awali alikuwa Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents