Michezo
Liverpool yatinga fainali ya Capital One
klabu ya Liverpool imefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya Capital One Cup baada kupata ushindi wa penati 6-5 dhidi ya kikosi kigumu cha klabu ya Stoke City.
Beki Marc Muniesa ndiye aliyekosa penati ya mwisho ya Stoke baada ya kuokolewa na kipa Simon Mignolet, huku kiungo Joe Allen akifunga penati ya mwisho ya ushindi.
Liverpool wanasubiri mshindi wa mchezo mwingine wa nusu fainali unaochezwa leo kati ya Manchester City watakaokua katika uwanja wao wa Etihad wakiwaalika Everton.
Everton wanaongoza kwa ushindi wa mabao 2-1, waliyopata katika mchezo wa kwanza.