Habari

Story kuwa serikali ya Eritrea imetoa amri wanaume kuoa wake wawili lasivyo kufungwa jela ni ya uongo

Bila shaka katika pita pita zako kwenye mitandao ya kijamii umekutana na picha za utani kuhusu wasichana warembo wa Eritrea na kwamba wanaume wa nchi zingine Afrika wanapanga kukata ndege kwenda nchini humo.

Utani huo ulianza baada ya mtandao wa SDEKenya kuandika habari kuwa serikali ya Eritrea imetoa amri kuwa wanaume wa nchi hiyo wanatakiwa kuoa wake wawili na wakikiuka watakabiliwa na kifungo jela.

Eritrea

Hata hivyo imebainika kuwa habari hiyo ni ya uongo. Ikumbukwe kuwa SDEKenya ndio website iliyozusha kuwa Magufuli amepiga marufuku uvaaji wa sketi fupi na kuifanya ikulu ya Dar es Salaam ikanushe uzushi huo.

Ukweli ni kwamba sheria ya Eritrea hairuhusu wanaume kuoa zaidi ya mke mmoja na kwamba kama mwanaume akifanya hivyo anaweza kufungwa jela miezi 6 au 12.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents