Habari

Maandamano ya kumpinga Waziri Mkuu Israel yapamba moto

Polisi ya Israel imesema imewakamata watu kadhaa leo Jumapili katika maandamano ya nchi nzima yaliovutia maelfu ya watu.

Israel: Many held in protests over gov't handling of coronavirus ...

Maandamano hayo yanafanyika kuonyesha kutoridishwa kwa jinsi Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu anavyolishughulikia janga la virusi vya Corona nchini humo.

Maelfu ya watu wameandamana nje ya nyumba ya Netanyahu mjini Jerusalem huku mamia ya wengine wakikusanyika mjini Tel Aviv wakishinikiza kujiuzulu kwa Waziri Mkuu huyo.

Kwenye mkutano na waandishi habari wiki iliyopita uliofanyika sambamba na maandamano hayo, Netanyahu aliwaonya waandamanaji hao dhidi ya kufanya uharibifu, ghasia na vurugu.Wakosoaji wanasema polisi wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi kuzima maandamano hayo. Hata hivyo, polisi inasema inawaondoa baadhi ya waandamanaji wanaovunja sheria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents