Burudani

MABESTE msanii anayekuja kwa kasi

Jamaa ni mkali ile mbaya kwa jina anaitwa William Ngowi lakini kwa jina la kisanii jamaa anajulikana kama Mabeste kutoka pande za B hits. Mshikaji tuko deep sana kiasi naweza sema akija kusikika hutojutia kumsikiliza tena na tena. Bongo5 haikua nyuma kumtafuta mitaa ya B hits chini ya producer wake Pancho latino. Jamaa anatokea pande za Kenya, Mombasa baada ya kukutana na Pancho latino na kugundua kipaji cha mshikaji pancho hakutaka kumuacha aite mbele yake bila kugusa kinanda na kutoa track ya inayokwenda kwa jina la Nawapenda wakati huo wako Dhahabu Records kwa mtu mzima Dully Sykes.

 

Mabeste akiwa Chini ya dhahabu records enzi zile haikua tu nawapenda but kama unakumbuka ile Dhabu Anthem track ambayo alikuwepo Dully Mwenyewe, Chidi Beenz, Chiku Ketto, MwanaFA, Mr Blue, Pia Mabeste akuishia hapo Jose Chamilion aliwahi kumtamani pia na wakafanya kazi pamojah.

Baada ya Pancho kutoka Dhahabu Ilibidi mabeste kurudi kenya kwa muda kwa sababu pancho hakutakiwa kuingia na msanii zaidi ya waliopo Kiri Records kipindi hicho.

Pancho hakudumu sana Kiri akaama B hits Groups kwa mtu mzima Hermy B ndipo Mabeste alipopata mwanya tena wa kurudi Bongo na hakusita kutoa track moja matata inayokwenda kwa jina la Nacheza Raff,ambayo haikuweza fanya vizuri, Pesa Iko wapi ambayo amemshirikisha Amani, Sukuma.

Na sasa Mabeste Ameachia Track yake mpya inyokwenda kwa jina la chupa Moja produza akiwa na Pancho latino toka B hits.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents