Michezo

Madrid yamtambulisha mrithi wa Ronaldo ndani ya Santiago Bernabeu (+video)

Katika hali isiyo ya kawaida klabu ya Real Madrid imemtambulisha rasmi mchezaji wake, Mariano Diaz aliyesajiliwa akitokea timu ya Lyon kuwa mrithi wa jezi namba saba iliyokuwa ikivaliwa na mshambuliaji hatari duniani ,Cristiano Ronaldo aliyesajiliwa na Juventus ya Italia.

Diaz mwenye umri wa miaka 25 amesajiliwa kwa dau la pauni milioni 18.6 akitokea Lyon ambapo alijiunga na klabu hiyo mwaka 2017 akitokea hapo hapo kwa mabingwa wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid.

Wachambuzi wa mambo wanaona kama ni hali isiyo kuwa ya kawaida kwa Madrid kumkabidhi kijana huyo jezi ya namba saba kutokana na aliyeiwacha kuifanyia makubwa ukilinganisha na Diaz ambaye wanaamini huwenda akashindwa kuitendea haki.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents