FahamuHabari

Mahakama ya Uganda yawatoza faini wanandoa wa Marekani kwa kumtesa mtoto wa kambo

Mahakama nchini Uganda imewaamuru wanandoa wa Marekani walioshtakiwa kwa kumtesa mtoto wao wa kambo kumlipa $26,000 (£20,700) kama fidia.

Fidia hiyo ilitokana na makubaliano ya rufaa, ambayo pia yaliifanya mahakama kuwafutia mashtaka ya biashara haramu ya ulanguzi na mateso dhidi ya wanandoa hao, jambo ambalo lingewafanya kupata kifungo cha maisha jela au kifo.

Wanandoa hao, Nicholas na Mackenzie Spencer walikamatwa mwaka jana na kushtakiwa kwa kumtesa mvulana huyo wa miaka 10 kwa kipindi cha miaka miwili.

Hii ni baada ya yaya wa mtoto huyo kuandikisha ripoti polisi akidai kuwa wanandoa hao walimtendea unyama mtoto huyo mara kwa mara.

Siku ya Jumanne, walikiri mashtaka ya unyanyasaji wa kikatili, unyama au udhalilishaji, kufanya kazi bila vibali na kukaa Uganda kinyume cha sheria, ambapo walitozwa faini ya shilingi za Uganda milioni 4.86.

Lakini uamuzi huo wa Jumanne umewakasirisha wanaharakati wa haki za watoto ambao walikiita “kejeli kwa haki”.

Mwanaharakati Proscovia Najjumba alihoji jinsi mahakama iliwaruhusu wanandoa hao “kuondoka” baada ya kukubali “walimtendea mtoto ukatili”, shirika la habari la AFP liliripoti.

Nyaraka za mahakama zilionyesha kwamba wanandoa hao walimpa mtoto chakula baridi, na kumfanya alale kwenye jukwaa la mbao lisilo na godoro .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents